Friday, March 1, 2013

Anguko yaingia post production

Short film ya iitwayo 'Anguko' sasa yaingia post production ikiwa ni kuhaririwa katika upande wa picha na sauti kwa maana ya Automated Dialogue Replacement, au Additional Dialogue Recording (ADR). "Ikiwa katika hatua hii tunamshukuru Mungu kwa kutufanikishia na tunatoa shukrani za dhati kwa wote walio shiriki na watakaoshiriki kwa namna moja au nyingine", Director alikaririwa akisema. Ukurasa huu unakuletea baadhi ya picha mbali mbali wakati wa kuchukua picha (shooting).

Director wa 'Anguko' Edgar Ngelela akielekeza jambo

Shooting ilikwenda vyema lakini kama kawaida havikosekani vitu vya kufurahisha. Kwa sababu ya upepo mkali wa baharini waliokuwa wakishika reflectors walipata taabu kidogo na wakati mwingine upepo uliwaelemea. Hapa kwenye picha ifuatayo Ally Hamoud akigombana na reflector kwenye upepo mkali

Ally Hamoud akitaabishwa na reflector
Anguko Imekuwa ikishootiwa na Salehe Khamis ambaye alikuwa akisaidiwa na Faraji Kakingo. Hapa katika picha inayofuata ni Salehe akiwa kazini na chini Faraji na Edgar Ngelela ambaye ni director wa filamu hiyo wakishuhudia moja ya tukio katika Camera.

Salehe Khamis akiwa kazini
Faraji Kakingo na Edgar Ngelela wakiwa nyuma ya Camera
Shughuli ilikuwa pevu na kila mtu alijitahidi kujishughulisha. Katika picha ifuatayo Mustafa Masoud akiwa katika scene moja wapo ya 'Anguko'.

Mustafa Masoud akiwa kwenye moja ya scene
Mtu ambaye mara nyingi sana husahaulika ni mtu wa make up. Katika picha ifuatayo dada wa make up ambaye pia ndiye production manager wa filamu hiyo akifanya kazi yake.

Happiness Mtuya Akimfanyia Make up Mustafa Masoud
Kwenye lights hakuwapo Ally Hamoud peke yake bali alikuwa akiwasaidia Yassin Ndossi na Inocent Justin. Picha ifuatayo vijana wakiwa kazini kuhakikisha swala la mwanga limedhibitiwa.

Inocent Justin na Ally Hamoud wakiwa wameshika reflactors
Kati ya watu muhimu waliokuwa wakimsaidia Director katika michakato na mipango mbali mbali ni Nimesh Vara na Smith Kimaro. Picha inayofuata Smith akionesha picha mbali mbali alizowapiga wasanii wakiwa kazini kwenye location. Hata nyingi ambazo zimaonekana hapo juu ni kazi ya Smith Kimaro.

Smith akiwaonesha wasanii picha mbali mbali alizopiga wakati wa shooting
Picha inayofuata Janet akijiandaa kuanza shooting ya Scene. Pembeni yake ni Happiness Mtuya akiwa kazini kuhakikisha yuko tayari.

Janeth Lameck akiwa kwenye moja ya scene za 'Anguko'
Asilimia kubwa ya waliogiza na kujihusiha kama crew ni wanafunzi wa Tanzania film training center (TFTC). Wote walijitahidi walivyoweza wengi wao wakiomba filamu hii iwainue mbali hasa wakilifikiria tamasha la filamu la Zanzibar International film festival (ZIFF).





No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...