Friday, February 8, 2013

"Anguko" yaingia location

Filamu fupi ambayo ambayo kwa sasa imepewa jina la 'Anguko-The fall' (Jina likiwa bado liko kwenye majadiliano) Imeingia location leo. Ikisimamiwa na Keen Insight production wakishirikiana na Born again films production pamoja na Tanzania film trainning Center (TFTC) Filamu hii inategemewa kuwa na urefu wa dakika tano (5).

Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye production ya Anguko
Kiongozi (Director) wa Filamu hii bwana Edgar Ngelela akizungumza na blog hii alisema "Kama ilivyozoeleka kusikika, mabadiliko yanaanza na wewe, mimi na kila mmoja wetu, nimeona ni vyema kazi ianze sasa."

Mmoja wa wahusika Faraji Kakingo akiwa location
Edgar aliendelea kusema kuwa katika filamu hii kajaribu kupunguza vitu vingi na kujaribu kuongeza usanii katika kazi. Alisema kuwa likiachwa swala la muda hata wahusika nao wapo wachache, yaani sita (6) peke yake. "Tunategemea kumaliza Production ya filamu hii mwishoni mwa mwezi huu wa pili," Edgar alimalizia.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...