Friday, March 1, 2013

Anguko yaingia post production

Short film ya iitwayo 'Anguko' sasa yaingia post production ikiwa ni kuhaririwa katika upande wa picha na sauti kwa maana ya Automated Dialogue Replacement, au Additional Dialogue Recording (ADR). "Ikiwa katika hatua hii tunamshukuru Mungu kwa kutufanikishia na tunatoa shukrani za dhati kwa wote walio shiriki na watakaoshiriki kwa namna moja au nyingine", Director alikaririwa akisema. Ukurasa huu unakuletea baadhi ya picha mbali mbali wakati wa kuchukua picha (shooting).

Director wa 'Anguko' Edgar Ngelela akielekeza jambo

Shooting ilikwenda vyema lakini kama kawaida havikosekani vitu vya kufurahisha. Kwa sababu ya upepo mkali wa baharini waliokuwa wakishika reflectors walipata taabu kidogo na wakati mwingine upepo uliwaelemea. Hapa kwenye picha ifuatayo Ally Hamoud akigombana na reflector kwenye upepo mkali

Ally Hamoud akitaabishwa na reflector
Anguko Imekuwa ikishootiwa na Salehe Khamis ambaye alikuwa akisaidiwa na Faraji Kakingo. Hapa katika picha inayofuata ni Salehe akiwa kazini na chini Faraji na Edgar Ngelela ambaye ni director wa filamu hiyo wakishuhudia moja ya tukio katika Camera.

Salehe Khamis akiwa kazini
Faraji Kakingo na Edgar Ngelela wakiwa nyuma ya Camera
Shughuli ilikuwa pevu na kila mtu alijitahidi kujishughulisha. Katika picha ifuatayo Mustafa Masoud akiwa katika scene moja wapo ya 'Anguko'.

Mustafa Masoud akiwa kwenye moja ya scene
Mtu ambaye mara nyingi sana husahaulika ni mtu wa make up. Katika picha ifuatayo dada wa make up ambaye pia ndiye production manager wa filamu hiyo akifanya kazi yake.

Happiness Mtuya Akimfanyia Make up Mustafa Masoud
Kwenye lights hakuwapo Ally Hamoud peke yake bali alikuwa akiwasaidia Yassin Ndossi na Inocent Justin. Picha ifuatayo vijana wakiwa kazini kuhakikisha swala la mwanga limedhibitiwa.

Inocent Justin na Ally Hamoud wakiwa wameshika reflactors
Kati ya watu muhimu waliokuwa wakimsaidia Director katika michakato na mipango mbali mbali ni Nimesh Vara na Smith Kimaro. Picha inayofuata Smith akionesha picha mbali mbali alizowapiga wasanii wakiwa kazini kwenye location. Hata nyingi ambazo zimaonekana hapo juu ni kazi ya Smith Kimaro.

Smith akiwaonesha wasanii picha mbali mbali alizopiga wakati wa shooting
Picha inayofuata Janet akijiandaa kuanza shooting ya Scene. Pembeni yake ni Happiness Mtuya akiwa kazini kuhakikisha yuko tayari.

Janeth Lameck akiwa kwenye moja ya scene za 'Anguko'
Asilimia kubwa ya waliogiza na kujihusiha kama crew ni wanafunzi wa Tanzania film training center (TFTC). Wote walijitahidi walivyoweza wengi wao wakiomba filamu hii iwainue mbali hasa wakilifikiria tamasha la filamu la Zanzibar International film festival (ZIFF).





Friday, February 8, 2013

"Anguko" yaingia location

Filamu fupi ambayo ambayo kwa sasa imepewa jina la 'Anguko-The fall' (Jina likiwa bado liko kwenye majadiliano) Imeingia location leo. Ikisimamiwa na Keen Insight production wakishirikiana na Born again films production pamoja na Tanzania film trainning Center (TFTC) Filamu hii inategemewa kuwa na urefu wa dakika tano (5).

Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye production ya Anguko
Kiongozi (Director) wa Filamu hii bwana Edgar Ngelela akizungumza na blog hii alisema "Kama ilivyozoeleka kusikika, mabadiliko yanaanza na wewe, mimi na kila mmoja wetu, nimeona ni vyema kazi ianze sasa."

Mmoja wa wahusika Faraji Kakingo akiwa location
Edgar aliendelea kusema kuwa katika filamu hii kajaribu kupunguza vitu vingi na kujaribu kuongeza usanii katika kazi. Alisema kuwa likiachwa swala la muda hata wahusika nao wapo wachache, yaani sita (6) peke yake. "Tunategemea kumaliza Production ya filamu hii mwishoni mwa mwezi huu wa pili," Edgar alimalizia.

Tuesday, February 5, 2013

Tanzania: Movie Makers Reminded of Professionalism

Edgar Ngelela presenting his topic (Snap by Faraji Kakingo)
THERE is what it takes locally to reach the required standards in making a good and professional movie. The problem is that people don't want to reach these standards, the Assistant Lecturer at the University of Dar es Salaam's School of Journalism and Mass Communication, Edgar Ngelela, said.
For the country's true potential to be seen, he maintains, there has to be a move away from approaching movie-making in a relaxed manner and the adoption of a more professional one by practitioners. Hearing these requirements for making a good movie brought the independent Beauty Consultant, Fidelis Madaha, to reality.

He told the 'Daily News' that he found the entire presentation challenging, because now he knew what it would take for him to move into the makeup section of a production crew on a film-set.
In fact, Ngelela's presentation, at the Arts Council's (BASATA) Jukwaa la Sanaa platform revealed to him the high degree of planning required before setting out shooting a film. Now Madaha fully understands why he will have to go back to study specifically for this area before he can stand a chance of fulfilling his dream. Ngelela had explained the three phases to making a movie. 
This was how Madaha came to understand the first phase, preproduction, has to be handled to an acceptable level before moving onto the production and postproduction ones respectively.

In conversation with the 'Daily News' after the presentation he explained that both members of his establishment and the weekly meeting organisers thought this topic suitable for this platform because they wanted to stimulate a change in the chain of local movie production.

"We had noticed that most people do not concentrate on the preproduction stage, but actually focus much on production. They don't know much about the preparation that will make the production to be something valuable to be watched.

So by the end of the day you see this level of Bongo movies where the graph is not coming up but remains stagnant and flat," Ngelela clarified. He directed those present, who wanted to take on this challenge to the Tanzania Film Training Centre (TFTC), here in Dar es Salaam, as the place where locals can be trained to be different actors, who bring out what a director wants them to.

There are mistakes which are made here that need to be ironed out first, he said, for the end product to be of a higher quality. Whereas he has no objection to radio plays, he does feel it's wrong to handle a film-set as if it's being broadcasted on the radio.

He finds that it is often forgotten in local circles that movies are based on action, so the emphasis is on what is being seen at a particular time and not what one imagines. "The script should not be like that of a radio. We have scripts that have a lot of dialogue, which makes them resemble something for radio, which you only have to listen to know what is happening.

On the screen you're not only listening, you're listening, while at the same time you're watching, so you're getting everything at the same moment. So there has to be a difference," he specified. On a personal level he has reduced the number of local movies he watches because of them being so limited.

He singled out the recently released "Chumo" as being one of the better local movies. Another is "Chungu" that has been done and cuts across the mistakes that are usually met in too many local productions, he finds.

Monday, February 4, 2013

Edgar Ngelela ndani ya Jukwaa la sanaa

Kama ilivyo ada leo tena wasanii kutoka sehemu mbalimbali za Dar es Salaam walikutana pale Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kusikiliza mada iliyokuwa imeandaliwa. Mada ilikuwa ni "Hatua muhimu za utengenezaji wa movie". Mada hii iliandaliwa na kuzungumzwa na Bw. Edgar Ngelela ambaye alisaidiana na Bw. Wilson Makubi ambaye ni Mratibu wa Tanzania Film Training Center (TFTC).

Edgar Ngelela Akitoa mada (Picha na Faraji Kakingo)
 Katika Mada hii Bw. Edgar alielezea hatua tatu muhimu ambazo ni; hatua ya maandalizi (Pre-production phase), hatua ya utengenezaji au uzalishaji (Production phase), na hatua ya uhariri na ukamilishaji (Post-production phase). Katika hatua hizi tatu Edgar aliendelea kueleza kwamba watu wengi wanaojishughulisha na kazi za utengenezaji wa movie wamejikita zaidi na wameweka nguvu yao yote katika hatua ya pili ya utengenezaji au uzalishaji  (Production phase).

Kabla ya kuanza kupokea maswali ya waliohudhuria Edgar Ngelela alimaliza kwa kueleza kuwa hatua muhimu ya kutilia maanani na kuweka nguvu kubwa ni hatua ya maandalizi (Pre-production phase). Alisema maandalizi yakifanywa vizuri kwa ufasaha kuna dalili zote za kufanya kazi nzuri au kutoa movie nzuri.

Thursday, December 27, 2012

Usiku Mtukufu-O holy (Tanzanian) night

Keen insights has released in the internet today a new music video production. The video is of the song O holy night. The song has been produced and Africanized by Ronald Nakaka at the Highland studios. The Camera work was done by Nicholas Calvin.


The video was Directed by Edgar Ngelela and Grace Nakaka. The video was an interesting project. The lighting was done with natural firewood light with a very dim little light just to support the fire in just some aspects for effect. The song 'Usiku Mtukufu was sang by Paul Mtaze and Gerald Nyiti.

Enjoy!



Friday, July 20, 2012

Timeless Tanzania

This is another Keen Insights production. It is a promotional video for the Pongo Safari's company on the services the company provides and the places to visit when one visits Tanzania, either towering or business in the wonderful breath taking "Timeless Tanzania". Check it out and Pongo Safari will be at your service.

Saturday, December 17, 2011

The 1st Chilren Arts Festival

Hatimaye tamasha la kwanza la watoto la sanaa (The first Arts Festival) lafanyika. Tamasha hili limefanyika leo hii tarehe 17/12/2011 kuanzia saa 9:00am -4:30pm. Tamasha hili lilihudhuriwa na watu mbali mbali na maonesho yalifana sana. Yafuatayo ni matukio katika picha.

Watoto wa TCTC Tabata wakiimba wimbo wa Bob Rudala katika Tamasha hilo.
Watoto wa Shada kutoka Bagamoyo wakionyesha Sarakasi.
Watoto wa friends of Don Bosco kutoka Kimara-Suka wakicheza Mganda
Ukumbi wa Nyumba ya utamaduni ulivyolipendezesha Tamasha
Mwenyekiti (Chairperson) Akifunga Tamasha

Mtoto wa KAOMU High view Nursery and Primary school kutoka Mbagala akipokea zawadi.
Na hawa ndio walikuwa wanakamati wa Tamasha hili la kwanza

Tamasha lilibarikiwa na Uwepo wa Bob Rudala mwenyewe Pamoja na wasanii wengine kama Raza na Vitalis Maembe.
Bob Rudala
Vitalis Maembe akiwa na Chanjo ya Rushwa

Tamasha liliahirishwa kwa mategemeo kufanyika tena mwakani mwaka 2012.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...