Kama ilivyo ada leo tena wasanii kutoka sehemu mbalimbali za Dar es Salaam walikutana pale Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kusikiliza mada iliyokuwa imeandaliwa. Mada ilikuwa ni "Hatua muhimu za utengenezaji wa movie". Mada hii iliandaliwa na kuzungumzwa na Bw. Edgar Ngelela ambaye alisaidiana na Bw. Wilson Makubi ambaye ni Mratibu wa Tanzania Film Training Center (TFTC).
Katika Mada hii Bw. Edgar alielezea hatua tatu muhimu ambazo ni; hatua ya maandalizi (Pre-production phase), hatua ya utengenezaji au uzalishaji (Production phase), na hatua ya uhariri na ukamilishaji (Post-production phase). Katika hatua hizi tatu Edgar aliendelea kueleza kwamba watu wengi wanaojishughulisha na kazi za utengenezaji wa movie wamejikita zaidi na wameweka nguvu yao yote katika hatua ya pili ya utengenezaji au uzalishaji (Production phase).
Edgar Ngelela Akitoa mada (Picha na Faraji Kakingo) |
Kabla ya kuanza kupokea maswali ya waliohudhuria Edgar Ngelela alimaliza kwa kueleza kuwa hatua muhimu ya kutilia maanani na kuweka nguvu kubwa ni hatua ya maandalizi (Pre-production phase). Alisema maandalizi yakifanywa vizuri kwa ufasaha kuna dalili zote za kufanya kazi nzuri au kutoa movie nzuri.
1 comment:
Doing what u do best bro. me loving all this.
Post a Comment