Katika
kumuenzi Marehemu Mzee Felix Ngelela Luhende wa Shinyanga anapofikisha miaka
minne (4) tangu mauti yake; familia yake ikiongozwa na Mama Hildegard Felix
Luhende ilijitoa na kusaidia watoto wasioona, wasiosikia na watoto wenye
ulemavu wa ngozi wa kituo cha Blinds kilichopo Buhangija - Shinyanga kwa kuweka
plasta na sakafu katika upande mmoja wa bweni moja ambalo lilikuwa
halijamaliziwa na bado halitumiki ipasavyo.
|
Bweni lililowekewa plasta na sakafu |
|
Bweni kabla ya ujenzi wa plasta na sakafu |
|
Bwenini: Ujenzi ukiendelea |
|
Bwenini: Baada ya ujenzi kukamilika |
Mpaka siku ya terehe 21/09/2014
kituo kilikuwa kina watoto 276 ambao wanachangia mabweni matatu; la nne likiwa
ndio hilo ambalo halijakamilika. Mabweni haya bado hayawatoshi watoto wote kwa
pamoja. Hii huwalazimu watoto hao kulala wawili wawili mpaka wanne wanne kwenye
kitanda kimoja.
|
Hivi ni vitanda ambavyo walemavu hulala wawili wawili mpaka wanne |
Ili
watoto waweze kuyatumia mabweni haya kwa ufasaha bweni mmoja lina uwezo wa
kuwahifadhi watoto 48 lakini kwa hali ya sasa bweni mmoja hubeba watoto 75
mpaka 80 na zaidi, jambo ambalo huwatisha walezi hasa wakifikiria magonjwa ya
mlipuko.
Hii
iliwafurahisha sana watoto wakitazamia muda si mrefu wengine kuhamia humo na
hivyo kupunguza kujaa kwenye mabweni mengine.
Zaidi
ya hapo familia ya Mzee Felix Luhende pia iligundua watoto hao walikuwa hawana
mahala pa kuanika nguo zao ambapo walilazimika kuanika nguo hizo kwenye
madirisha, hivyo familia ikaona ni vema kuwawekea watoto hao kamba kadhaa za
kuanikia nguo zao.
|
Chuma za kufungia kamba za kuanikia nguo zikisubiriwa kukauka |
Kituo bado kinahitaji sana
misaada mingi kama vile kusaidia kuboresha jiko lao ili kuruhusu hewa zaidi
kuingia ndani, kuboresha bwalo lao, kuongeza vitanda na magodoro, chakula na
kadhalika.
Zaidi ya hapo walezi wanahitaji mafunzo zaidi ya malezi na usimamizi
ili kuboresha baadhi ya mambo ya msingi katika kuwalea watoto hao.