Sunday, November 8, 2015

Karibu music festival 2015

Tamasha la pili la 'Karibu Music' laendelea kukonga nyoyo za mashabiki mara nyingine tena. Tamasha hili lililoanza siku ya Ijumaa tarehe 06/11/2015 linategemewa kuahirishwa tarehe 08/11/2015 siku ya Jumapili. Mwandishi wetu alisogea Bagamoyo katika viwanja vya Mwanakalenge kwenye tamasha hilo siku ya Jumamosi na kukutana na wasanii mbali mbali ambao walifanya kazi nzuri sana. Miogoni mwao alikuwako Jhiko Manyika, Damian Soul, H art the band na Papa Wemba. Unagana na mwandishi wetu kwa picha za tamashani:

The second "Karibu Music Festival' continues on its second day at the Mwanakalenge grounds in Bagamoyo. The Festival this year commenced on Friday 06/11/2015 and expected to go on for three days; till Sunday 08/11/2015. Our journalist was at the festival on Saturday and met a variety of celebrities who also performed. These included Jhiko Manyika, Damian Soul, H art the band and Papa Wemba. Join us to the Festival through the following snaps:

Brina from Jamaica performing at the 2nd  Karibu Music Festival 2015 

Damian Soul at the 2nd Karibu Music Festival 2015

Damian Soul's drummer Tito at the 2nd Karibu Music Festival 2015

Damian Soul's keyboard Artist Hary at the 2nd Karibu Music Festival 2015

Damian Soul's guitarist Emmanuel at the 2nd Karibu Music Festival 2015

Masafa at the 2nd Karibu Music Festival 2015

Damian Soul and his band at the 2nd Karibu Music Festival 2015

Damian Soul performing at the 2nd Karibu Music Festival 2015

Saxophonist at the 2nd Karibu Music Festival 2015

Jhiko Manyika at the 2nd Karibu Music Festival 2015 in Bagamoyo

Jhiko Manyika performing at the 2nd Karibu Music Festival 2015 in Bagamoyo

H art the band in Bagamoyo at the 2nd Karibu Music Festival 2015

An artist form the H art the band performing at the Karibu Music Festival 2015

An artist form the H art the band performing at the Karibu Music Festival 2015

An artist form the H art the band performing at the Karibu Music Festival 2015

An artist form the H art the band performing at the Karibu Music Festival 2015

H art the band in Bagamoyo performing at the 2nd Karibu Music Festival 2015

Papa Wemba in Bagamoyo at the 2nd Karibu Music Festival 2015

Papa Wemba in Bagamoyo performing at the 2nd Karibu Music Festival 2015

Tuesday, March 3, 2015

Filamu fupi ya 'KOSA' yaingia production.

Mwongoza na mtayarishaji mahiri wa Filamu hapa nchini Edgar Ngelela anatarajiwa kuachia filamu mpya fupi iliyopewa jina la ‘KOSA’ mwanzoni mwa mwezi wa nne mwaka huu.

Filamu mpya ya 'KOSA'
Ngelela ambaye filamu yake ya awali ya ‘Anguko’ ilipata mafanikio makubwa ya kuoneshwa katika tamasha la kimataifa la 16 la majahazi (ZIFF) huko Zanzibar mwaka 2013, ameiambia Radio Mlimani kwamba filamu hiyo fupi ya ‘KOSA’ inatarajiwa kuwa na urefu wa dakika 25 ikizungumzia maisha ya kila siku.

“Maudhui ya filamu yangu mpya ni maisha ya kila siku lakini zaidi inagusa mapezi, imani na mazoea” alisema Ngelela wakati akizungumza na Radio Mlimani juu ya ujio wa filamu hiyo mpya.

Ngelela ameamua kuiita filamu hiyo ‘KOSA’. Neno hilo la Kiswahili limeubeba ujumbe wa filamu hiyo ipasanyo; kwanza limetumika katika filamu hii likimaanisha kukosa, lakini pia limetumika likimaanisha kukosea, hivyo basi neno hilo limebeba mambo yote mawili katika filamu hiyo fupi, Ngelela alisema.

“Filamu hii ni filamu inayotoa ujumbe kwamba kama mwanadamu ni lazima uwe makini katika kufanya maamuzi, lakini pia kuwaambia watanzania kwamba kila mahusiano ya kimapenzi yana upekee wake” alimalizia mtayarishaji huyo.

Filamu hiyo itakayokamilika mwanzoni mwa mwezi wa nne imelengwa kuoneshwa katika matamasha mbalimbali ya kimataifa na vile vile itapatikana katika DVD hapo baadae.

Miongoni mwa nyota wa filamu hapa nchini waliongára katika filamu hiyo ni pamoja na Bi Madina Hamis maarufu kama dada zawadi pamoja na Emmanuel Myamba anayejulikana zaidi kama Pastor Myamba. Wapo pia waigizaji chipukizi ambapo kwa mujibu wa Ngelela wamefanya kazi kubwa katika filamu hii.

Filamu hiyo imechezewa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na pia katika viunga vya mji wa Morogoro.


Na Sylvia Mwehozi, Radio Mlimani.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...